MAGNESIUM PHOSPHIDE ICSC: 0744
Machi 1998

Trimagnesium diphosphide
CAS # 12057-74-8 Mg3P2 / Mg=P-Mg-P=Mg
RTECS # OM4200000 Masi ya molekuli: 134.9
UN # 2011
EC # 015-005-00-3
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki lakini hutengeneza gesi inayoungua ikigusana na maji au hewa nyevunyevu. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na maji.
dioksidi kaboni, mchanga mkavu, USITUMIE maji.
MLIPUKO Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na maji au hewa yenye unyevunyevu.


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MFIDUO KWA VIJANA NA WATOTO!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Maumivu ya tumbo. Mchomo. Kikohozi. Kizunguzungu. Mazimbwezimbwe. Kuumwa kichwa. Kupumua kwa shida. Kichefuchefu. Kuumwa koo.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Degedege. Kuhara. Kupoteza fahamu. Kutapika. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo vinavyokalafatika. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linaloruhusu gesi linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: F, T+
R: 15/29-28
S: (1/2-)-22-43-45
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 4.3
Jasara tanzu za UN: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 43G15
Isodhurika kwa moto. Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Hifadhi katika vyombo vikavu, vilivyofungwa, vilivyotandwa plastiki (poliethilini). Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Tazama Hatari za Kikemikali. Kavu. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
MAGNESIUM PHOSPHIDE ICSC: 0744
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE MANJANO HADI KIJANI

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu kama vile oksidi za fosforasi na fosjini, ambayo huongeza athari ya moto. Humenyuka pamoja na maji na hewa yenye unyevunyevu, kwa ukali sana pamoja na asidi, kutoa fosjini kusababisha athari ya moto na yenye sumu.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi poda au vumbi, na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho na njia ya upumuaji. Tazama Vidokezo.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: >750°C
Uzito wiani: 2.1 g/cm³
Umumunyifu katika maji: mmenyuko
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii huingia katika mazingira kwa matumizi ya kawaida. Utaratibu wa hali ya juu lazima unahitajika ili kuzuia kiasi zaidi kisitokee kama kupitia kwa kutupwa ovyo.
VIDOKEZO
Humenyuka kwa nguvu na vitenzi vya kuzimia moto kama vile maji. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Detiaphos, Mag-disc, Magtoxin, Phostoxin ni majina ya kibiashara. Ona ICSC 0694 (Phosphine).
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005