| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka. Michanganyiko ya vioevu vyenye vimumunyisho vya kaboni huweza kuwaka (moto). Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto.
|
Povu linalokinza alkoholi, poda, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
|
|
|
| MFIDUO |
|
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU! EPUKA MFIDUO KWA VIJANA NA WATOTO!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
(Tazama Kumeza).
|
Kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA!
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Miwanivuli ya usalama, au kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Kuchanganyikiwa. Degedege. Kichefuchefu. Kutapika.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia).
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi kikali cha maji/bahari. Ainisho ya EU Alama: Xn, N R: 21/22-40-50/53 S: (2-)-36/37-60-61 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G41c.
|
Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho, besi na maunzi yasiokubaliana: Tazama Hatari za Kikemikali. Kilichofungwa vizuri. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KITEKINIKALI: MANJANO ISIYOKOZA HADI MANJANO-KAHAWIA, KINATACHO HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapochomwa, inapogusana na besi huzalisha mafusho yenye sumu kama vile klorini, fosjini, kloridi hidrojeni. Hushambulia feri, zinki, plastiki, mpira na mipako. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: ppm; 0.5 mg/m³ (kama TWA), A3 (ngozi) (ACGIH 1997) |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka wakati wa kunyunyiza. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Mfiduo wa viwango vya juu huweza kuleta kichanganyikiwa, kutetemeka, degedege, matatizo ya kupumua na kifo. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Dutu hii huweza kuathiri ini na mfumo kinga, kusababisha vidonda vya tishu na kuharibika kwa ini. Dutu hii ina uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko ifikapo 0.27kPa: 175°C Uzito wiani (maji = 1): 1.59-1.63 Umumunyifu katika maji: hakuna Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 25°C: 0.0013 |
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.78 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa viumbe viishivyo ardhini, nyuki. Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira kwa sababu hubakia kwenye mazingira. Dutu hii inaweza kusababisha madhara yatakayoonekana baadaye katika mazingira ya maji.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Angalia pia kadi ya viyeyusho endapo vimetumiwa kutengenezea dutu hii. Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za kitoksini. Belt, Chlor Kil, Chlortox, Corodan, Gold Crest, Intox, Kypchlor, Niran, Octachlor, Sydane, Synklor, Termi-Ded, Topiclor na Toxichlor ni majina ya kibiashara. Pia shauriana na ICSC #0743 (Heptachlor).
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||