TIN (II) CHLORIDE DIHYDRATE ICSC: 0738
Aprili 2004

Stannous chloride dihydrate
CAS # 10025-69-1 SnCl2. 2H2O
RTECS # XP8850000 Masi ya molekuli: 225.6
UN # 3260
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO


Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kuhara. Kichefuchefu. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 8
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 80GC2-II+III
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
TIN (II) CHLORIDE DIHYDRATE ICSC: 0738
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
MANGO KATIKA MAUMBO MBALIMBALI ISIYO NA RANGI HADI NYEUPE

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Inapokanzwa, hutoa mafusho yenye sumu. Dutu hii ni kinakisishaji kikali na humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: (kama Sn, oksidi na misombo isokikaboni, isipokuwa hidridi ya bati) 2 mg/m³ kama TWA; (ACGIH 2004).
EU OEL: (misombo isokikaboni ya bati, kama Sn) 2 mg/m³ kama TWA; (EU 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Kikolezo cha chembechembe ya dhuru yaweza kufikiwa haraka ikitawanywa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho na njia ya upumuaji.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Hutengana chini ya kiwango mchemko ifikapo 652°C
Kiwango myeyuko: 38°C
Uzito wiani: 2.71 g/cm³
Umumunyifu katika maji: vizuri sana (>100 g/100 ml ifikapo 20°C)
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Kiwango myeyuko dhahiri kinachosababishwa na upoteaji wa maji fuwele kimeelezwa. Stannochlor ni jina la kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005