4-VINYL TOLUENE ICSC: 0735
Aprili 1997

p-Methyl styrene
1-Ethenyl-4-methylbenzene
p-Vinyl toluene
CAS # 622-97-9 CH3C6H4CH=CH2 / C9H10
RTECS # WL5076000 Masi ya molekuli: 118.2
UN # 2618
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua. Ukanzaji unaweza kusababisha ongezeko la kanieneo na kuleta athari ya kupasuka.
Usiwashe moto.
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 52.8°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 52.8°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!

Kuvuta pumzi Kizunguzungu. Kusinzia. Mazimbwezimbwe. Kuumwa kichwa. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Ngozi kavu. Wekundu.
Glavu za kinga.
Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu.
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kichefuchefu. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Msimbo wa NFPA: H 2; F 2; R 2;
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi kali. Kilichofungwa vizuri. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri. Hifadhi iwapo tu imetulia.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
4-VINYL TOLUENE ICSC: 0735
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii huweza kupolimisha kutokana na kupata joto kwa athari ya moto au mlipuko. Humenyuka ikiwa na vioksidishaji vikali na asidi kali.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 50 ppm; 242 mg/m³ (kama TWA);
100 ppm; 483 mg/m³ (kama STEL) (ACGIH 1996)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Kioevu hukausha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri ini na mafigo kusababisha vidonda vya tishu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 173°C
Kiwango myeyuko: -34°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.897
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: <0.1
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.1
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.00
Kiwango cha kumweka: 52.8°C
Jotoridi la kujiwasha: 515°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.1-5.3
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 3.580
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Ona ICSC 0514 Mchanganyiko wa vinili toluini isoma.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005