| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua sana. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 16°C.
|
Mfumo funge wa zaidi ya 16°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kizunguzungu.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko.
|
| Ngozi |
Wekundu. Maumivu.
|
Glavu za kinga.
|
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Miwani ya usalama.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni).
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari. Ainisho ya EU Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 3 Jasara tanzu za UN: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30G32
|
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho, vioksidishaji, asidi, besi, alumina. Baridi. Kilichofungwa vizuri. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha kloridi hidrojeni na fosjini. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki. |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 120°C Kiwango myeyuko: -99°C Uzito wiani (maji = 1): 1.19 Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 0.3 Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 2.4 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.9 |
Kiwango cha kumweka: 16°C o.c. Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: tazama Vidokezo Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.0 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Vikomo vya ulipukaji havijulikani katika maandiko, japokuwa dutu hii inaweza kuwaka na ina kiwango cha kumweka pungufu ya 61°C. Hakuna data za kutosha kuhusu athari za dutu hii kwa afya ya binadamu kwa hiyo kunahitajika uangalifu mkubwa.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||