POTASSIUM PERCHLORATE ICSC: 0714
Novemba 2003

Potassium hyperchlorate
Perchloric acid, potassium salt
Peroidin
CAS # 7778-74-7 KClO4
RTECS # SC9700000 Masi ya molekuli: 138.5
UN # 1489
EC # 017-008-00-5
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki lakini huongeza mwako wa dutu nyingine. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na dutu ziwakazo.
Moto unapotokea katika eneo: maji mengi, mnyunyizio wa maji.
MLIPUKO
USIACHE kikaathiriwa na msuguano au mshtuko.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Osha salio kwa maji mengi. Usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru.
Ainisho ya EU
Alama: O, Xn
R: 9-22
S: (2-)-13-22-27
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 5.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 51S1489
Msimbo wa NFPA: H 1; F 0; R 2; ox
Kinachotenganishwa na dutu zenye kuungua na za kunakisi. Tazama Hatari za Kikemikali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
POTASSIUM PERCHLORATE ICSC: 0714
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE ISO RANGI AU PODA FUWELE NYEUPE

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi (klorini, oksidi za klorini). Dutu hii ni kioksidishaji madhubuti na humenyuka iwapo na maunzi yanayoweza kuwaka na yanayonakisi, kusababisha athari ya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri damu kusababisha kufanyika kwa methemoglobini. (Tazama Vidokezo).
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko (hutengana): 400°C
Uzito wiani: 2.5 g/cm³
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 1.8
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Haitahimili mshtuko ikiingiwa na misombo kikaboni. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005