DECABORANE ICSC: 0712
Oktoba 1997

Boron hydride
Decaboron tetradecahydride
CAS # 17702-41-9 B10H14
RTECS # HD1400000 Masi ya molekuli: 122.2
UN # 1868
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto. Usigusishe na halojeni, vioksidishaji.
Poda maalum, mchanga mkavu, USITUMIE kitenzi kingine.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 80°C. Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
Mfumo funge wa zaidi ya 80°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji.
MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kizunguzungu. Kusinzia. Kuumwa kichwa. Kutokwa jasho. Kichefuchefu. Kuumwa koo. Udhaifu. Kutetemeka. Kukosa mwelekeo. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Uingizaji hewa (hapana kama ni poda), mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. (Tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu.
Kingao cha uso.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 4.1
Jasara tanzu za UN: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Msimbo wa NFPA: H 3; F 2; R 1;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho, halojeni na vioksidishaji vingine. Baridi. Kavu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
DECABORANE ICSC: 0712
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE ISO RANGI HADI NYEUPE YENYE HARUFU KALI.

HATARI KWA MWILI:
Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Huweza kulipuka wakati wa kukanza au inapogusana na mialimoto. Dutu hii hutengana polepole inapokanzwa ifikapo 300°C kutoa boroni na gesi inayoweza kuwaka/kulipuka (hidrojeni ICSC001), na inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu (oksidi boroni). Humenyuka kwa upole na halojeni ya dutu hii na etha kutoa dutu inayosikia shindo. Yaweza kupasuka ikikuswa na vioksidishaji. Humenyuka pamoja na maji au unyevu kutoa gesi inayoweza kuwaka/kulipuka (hidrojeni ICSC001). Hushambulia mpira, raba isiyoasili (synthetic rubber), grisi na kiasi ya kulainisha.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.05 ppm; 0.25 mg/m³ (kama TWA);
0.15 ppm; 0.75 mg/m³ (kama STEL) (ngozi) (ACGIH 1997)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Erosoli hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva kusababisha kuchoka, kusumbuka na kusikia uzingisi. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva kusababisha uchovu, kutostamili na kukosa mwelekeo.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 213°C
Kiwango myeyuko: 99.6°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.9
Umumunyifu katika maji: kidogo kwa maji baridi; huyeyuka kwa maji moto
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 25°C: 6.65
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.2 (ifikapo kiwango mchemko)
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.00
Kiwango cha kumweka: 80°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 149°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: see Notes
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Dalili hazijitokezi mpaka baada ya masaa 24 hadi 48. Vikomo vya ulipukaji havijulikani katika maandiko, japokuwa dutu hii inaweza kuwaka na ina kiwango cha kumweka pungufu ya 61°C. Humenyuka kwa nguvu na vitenzi vya kuzimia moto kama vile haloni. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005