| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na maji.
|
Poda maalum, USITUMIE maji. USITUMIE vitenzi vingine.
|
| MLIPUKO |
Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na dutu za kuwaka na maji.
|
|
Utokeapo moto: poza mapipa n.k. kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji.
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Mchomo. Kikohozi. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi. Kuumwa koo. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Wekundu. Mibabuko ya ngozi. Maumivu. Malengelenge.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
|
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Msokoto wa tumbo. Maumivu ya tumbo. Mchomo. Kichefuchefu. Mshtuko au kuzimia. Kutapika. Udhaifu.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Mpeleke kwa daktari. Tazama Vidokezo.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Shauriana na mtaalam. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Fagia dutu iliyomwagika na kutia kwa vyombo vikavu, vya metali, vinavyoweza kufungwa. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Kisichoingiza hewa. Ainisho ya EU Alama: F, C R: 14/15-34 S: (1/2-)-8-43-45 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 4.3 Kikundi Ufungashaji cha UN: I | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 750 Msimbo wa NFPA : H 3; F 2; R 2; W |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi, haloni na nyenzo zingine sizilolingana. Tazama Hatari za Kikemikali. Kavu. Weka chini ya oili madini.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: METALI FEDHA-NYEUPE, LAINI. HUGEUKA MANJANO INAPOFIDULIWA NA HEWA NA UNYEVU. HATARI ZA KIKEMIKALI: Kukanza kunaweza kusababisha mwako au mlipuko mkali. Dutu hii huweza kuwaka yenyewe ikiguza hewa. Inapokanzwa, hutoa mafusho yenye sumu. Humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji vikali, asidi na misombo mingi (mwambatano haidrokaboni, halojeni, haloni, saruji, mchanga na asbesto) kusababisha athari ya moto na mlipuko. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na maji, kutoa hidrojeni, gesi inayoweza kuwaka/kulipuka, na mafusho babuzi ya hidroksidi lithiamu. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa. Kuvuta pumzi yenye dutu hii kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 1336°C Kiwango myeyuko: 180.5°C Uzito wiani: 0.5 g/cm³ Umumunyifu katika maji: mmenyuko (kwa ukali sana) Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 723°C: 133 |
Jotoridi la kujiwasha: 179°C | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya mnyunyuzio mwafaka unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||