FONOFOS ICSC: 0708
Aprili 1997

O-Ethyl S-phenylethylphosphonodithioate
CAS # 944-22-9 C5H5SPSCH2CH3OCH2CH3 / C10H15OPS2
RTECS # TA5950000 Masi ya molekuli: 246.3
UN # 3018
EC # 015-091-00-2
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Michanganyiko ya vioevu vyenye vimumunyisho vya kaboni huweza kuwaka (moto). Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Povu, poda, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU! EPUKA MFIDUO KWA VIJANA NA WATOTO!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Msongo/mfinyo (wa jicho), kukakamaa kwa msuli, utokaji mate kwa wingi. Kutokwa jasho. Kichefuchefu. Kizunguzungu. Kupumua kwa shida. Degedege. Kupoteza fahamu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Kioevu au erosoli vyaweza kufyonzwa. Wekundu. Maumivu. Kiwaa.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Udhaifu. Msokoto wa tumbo. Kutapika. Kuhara. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi kikali cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: T+, N
R: 27/28-50/53
S: 1/228-36/37-45-60-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G44
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
FONOFOS ICSC: 0708
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, ANGAVU, CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hidrolisisi hufanywa na asidi kali na alkali.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: ppm; 0.1 mg/m³ (kama TWA) (ngozi) (ACGIH 1996)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi, macho na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka wakati wa kunyunyiza.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Kizuizi cha kolinesterasi. Mfiduo zaidi ya OEL huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Kizuizi cha kolinesterasi; uwezekano wa madhara yake kulimbikizana: tazama athari za papo hapo/dalili.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko ifikapo 0.013kPa: 130°C
Kiwango myeyuko: 30°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.16
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 25°C: 0.03
Kiwango cha kumweka: 94°C c.c.
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 3.94
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa nyuki na viumbe hai vya majini. Epusha kuingia katika mazingira tofauti na matumizi ya kawaida.
VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Dalili za madhara ya sumu ya papo hapo hazijitokezi mpaka masaa kadhaa yamepita. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za kitoksini. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Difonate, Dyfonate 2G, na Stauffer N 2790 ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005