| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usigusishe na maji.
|
USITUMIE vitenzi vya majimaji. USITUMIE maji. Moto unapotokea katika eneo: poda, dioksidi kaboni na mchanga mkavu.
|
| MLIPUKO |
|
|
Utokeapo moto: poza mapipa n.k. kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji.
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Kuumwa koo. Kikohozi. Mchomo. Kichefuchefu. Kutapika. Kukosa pumzi. Kupumua kwa shida. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Maumivu. Wekundu. Malengelenge. Mibabuko ya ngozi.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Maumivu. Wekundu. Kutoa machozi. Kuungua kunakopenya sana. Upofu.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Mchomo. Maumivu ya tumbo. Mshtuko au kuzimia. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga mkavu au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia).
|
Kisichoingiza hewa. Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Alama: C R: 34-37 S: (1/2-)-7/8-26-45 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Jasara tanzu za UN: 8 Kikundi Ufungashaji cha UN: I | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 81 Msimbo wa NFPA: H 3; F 0; R 2; W |
Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Tazama Hatari za Kikemikali. Kavu. Kilichofungwa vizuri. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI AU MANJANO, KIFUKACHO CHENYE HARUFU KALI. HATARI KWA MWILI: Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi kama vile kloridi hidrojeni na oksidi za fosforasi. Humenyuka ikiwa na vioksidishaji. Humenyuka kwa nguvu na maji ikitoa joto na uchanganusi kama asidi hidrokloriki na asidi fosforiki, kusababisha athari ya moto na mlipuko. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na alkoholi, fenoli na besi. Hushambulia metali na dutu nyingine nyingi. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV (kama TWA): 0.2 ppm; 1.1 mg/m³ ; kama STEL: 0.5 ppm; 2.8 mg/m³ (ACGIH 1997) |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi au kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi wa mvuke wake kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Mfiduo zaidi ya OEL huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 76°C Kiwango myeyuko: -112°C Uzito wiani (maji = 1): 1.6 Umumunyifu katika maji: mmenyuko Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 21°C: 13.3 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.75 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.5 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Humenyuka kwa nguvu na vitenzi vya kuzimia moto kama vile maji. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||