FORMALDEHYDE (37% SOLUTION, methanol free) ICSC: 0695
Oktoba 2004

Methanal
Formalin
CAS # 50-00-0 H2CO
RTECS # LP8925000 Masi ya molekuli: 30.0
UN # 2209
EC # 605-001-00-5
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka.
Usiwashe moto.
Maji mengi, mnyunyizio wa maji.
MLIPUKO


MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!

Kuvuta pumzi Mchomo. Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kukosa pumzi.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Kutoa machozi. Wekundu. Maumivu. Kiwaa.
Kingao cha uso au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Mchomo. Kichefuchefu. Mshtuko au kuzimia.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Vazi linalokinga kemikali. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
Ainisho ya EU
Alama: T
R: 23/24/25-34-40-43
S: (1/2-)-26-36/37/39-45-51
Angalia: [B, D]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 8
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 80S2209
Msimbo wa NFPA: H 2; F 2; R 0;
Baridi. Kilichofungwa vizuri. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
FORMALDEHYDE (37% SOLUTION, methanol free) ICSC: 0695
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Humenyuka pamoja na asidi, metali za alkali na vioksidishaji vikali.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.3 ppm (kiwango cha juu); A2; SEN; (ACGIH 2004).
MAK: 0.3 ppm 0.37 mg/m³; kuhisisha ngozi (Sh); Aina ya kiwango cha juu: I(2); Aina ya sarakani: 4; Aina inayoleta mabadiliko kwa seli za uzazi: 5; Kundi la waja wazito lililo hatarini: C; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera kwa ukali macho, ngozi na inakera njia ya upumuaji.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Kuvuta hewa kwa kurudia au muda mrefu huweza kusababisha pumu-dalili kama pumu. Dutu hii husababisha kansa kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 98°C
Umumunyifu katika maji: vizuri sana
Kiwango cha kumweka: 83°C c.c.
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Ongezeko la kiimarishaji (methanoli) huweza kuathiri tabia ya kitoksini za dutu hii. Tazama ICSC 0057 Methanol. Kikomo thamani cha mfiduo matumizi ya kazi kisivukwe wakati wowote wa mfiduo amilifu.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005