ACRYLIC ACID ICSC: 0688
Oktoba 1997

Ethylenecarboxylic acid
Acroleic acid
2-Propenoic acid
CAS # 79-10-7 C3H4O2 / CH2=CHCOOH
RTECS # AS4375000 Masi ya molekuli: 72.07
UN # 2218 (imezuiwa)
EC # 607-061-00-8
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Mnyunyizo wa maji, povu linalokinza alkoholi, poda, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 54°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 54°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka. Mafusho hayatazuilika na yanaweza kujipolimisha ndani ya vitolea hewa chafu, na kuwepo hatari ya kuvunjika.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU! EPUKA MGUSANO WOWOTE!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo. Mchomo. Kukosa pumzi. Kupumua kwa shida. Inababua. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Malengelenge. Maumivu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana. Upofu.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Mchomo. Udhaifu. Msokoto wa tumbo. Kuhara. Mshtuko. Inababua. Kupoteza fahamu.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam endapo mwagiko ni mkubwa. Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vyenye lebo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Yaweza kuhifadhiwa kwenye vyombo vya kioo, chuma cha pua, alumini au vilivyotandwa poliethilini.
Ainisho ya EU
Alama: C
R: 10-34
S: (1/2-)-26-36-45
Angalia: [D]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 8
Jasara tanzu za UN: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 706
Msimbo wa NFPA : H 3; F 2; R 2;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, besi kali, asidi kali, vyakula na malisho. Weka gizani. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri. Usiruhusu igande ubadiridi. Hifadhi iwapo tu imetulia. (Tazama Vidokezo).
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ACRYLIC ACID ICSC: 0688
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa. Mchanganyiko wa mafusho na hewa hulipuka.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hupolimisha mapema kutokana na kukanza, kwa kuathiriwa na mwanga, oksijeni, vioksidishaji kama vile peroksidi au vitendaji vingine (asidi, chumvi za feri), kwa athari ya moto au mlipuko. Inapokanzwa, hutoa mafusho yenye sumu. Dutu hii ni asidi kali ya kati. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na besi kali na amini. Hushambulia metali nyingi, kujumuisha nikeli na shaba.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV (kama TWA): 2 ppm; 5.9 mg/m³ A4 (ngozi) (ACGIH 1997)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kupitia katika ngozi na kwa kumeza.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Hubabua. Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa. Kuvuta pumzi kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Athari zinaweza kuchelewa.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 141°C
Kiwango myeyuko: 14°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.05
Umumunyifu katika maji: kuchanganyika
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 413
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.5
Kiwango cha kumweka: 54°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 360°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 2.4-8
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.36 (imekadiriwa)
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Kiwango kidogo cha oksijeni hupunguza nguvu ya kizuizi, kusababisha hali hatari ya upolimishaji. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya mnyunyuzio mwafaka unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Usiiyeyushe baada ya kukandishwa kwa sababu dutu hii simadhubuti. Ongezeko la kiimarishaji au kiviza huweza kuathiri tabia ya kitoksini za dutu hii. Shauriana na mtaalam.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005