TRIFLUOROCHLOROETHYLENE ICSC: 0685
Machi 2002

Chlorotrifluoroethylene
Trifluorovinyl chloride
(silinda)
CAS # 79-38-9 C2ClF3
RTECS # KV0525000 Masi ya molekuli: 116.47
UN # 1082
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Funga ugavi; kama haiwezekani na hakuna hatari kwa mazingira, acha moto uwake hadi ujizime; ama sivyo zima kwa kutumia mnyunyizio wa maji, povu linalokinza alkoholi, poda kavu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 27°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 27°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka. Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza).
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO


Kuvuta pumzi Kizunguzungu. Kichefuchefu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
Glavu za kuhami baridi.
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo.
Macho
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.

KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Ondoa mvuke kwa mnyunyuzio mwembamba wa maji. (Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 2.3
Jasara tanzu za UN: 2.1

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20G2TF
Msimbo wa NFPA: H -; F 4; R 0;
Isodhurika kwa moto. Baridi.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
TRIFLUOROCHLOROETHYLENE ICSC: 0685
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
GESI ISO RANGI, ISO HARUFU

HATARI KWA MWILI:
Gesi hii huchanganyika vema na hewa, mchanganyiko unaolipuka hutokea kwa urahisi.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Inapowaka hutengeneza gesi babuzi na zenye sumu kama vile kloridi hidrojeni (ICSC 0163) na floridi hidrojeni (ICSC 0283).

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Kioevu hiki huweza kusababisha jamidi. Dutu hii huweza kuathiri mafigo.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: -28°C
Kiwango myeyuko: -158°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.3
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 25°C: 612
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.02
Kiwango cha kumweka: 27.8°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 24-40.3
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa mgongano kwa kanda ya ozoni.
VIDOKEZO
Ongezeko la kiimarishaji au kiviza huweza kuathiri tabia ya kitoksini za dutu hii, shauriana na mtaalam.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005