THEOPHYLLINE ICSC: 0678
Septemba 1993

3,7-Dihydro-1,3-dimethyl-1H-purine-2,6-dione
1,3-Dimethylxanthine
CAS # 58-55-9 C7H8N4O2
RTECS # XH3850000 Masi ya molekuli: 180.2
UN #
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi (Tazama Kumeza).
Epuka kuvuta pumzi yenye vumbi laini au ukungu.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Degedege. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kutapika. Enye harara. Kukosa uzingizi.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Kinachotenganishwa na vyakula na malisho.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
THEOPHYLLINE ICSC: 0678
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
PODA FUWELE ISO RANGI, NYEUPE

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu kama vile oksidi za nitrojeni.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa moyo na mishipa, mfumo mkuu wa neva, ini.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii huenda ikasababisha athari za sumu kwa uzazi na kukua kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: 270-274°C
Umumunyifu katika maji, g/100 ml: wastani
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -0.02 (imekadiriwa)
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Accurbrom, Bilordyl, Bronchorectard, Elixicon, Lasma, Sabidal, Theochram, Xanthium ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005