NAPHTHALENE ICSC: 0667
Aprili 2005

Naphthene
CAS # 91-20-3 C10H8
RTECS # QJ0525000 Masi ya molekuli: 128.18
UN # 1334 (mango); 2304 (myeyuko)
EC # 601-052-00-2
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka.
Usiwashe moto.
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 80°C. Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.

MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi Kuumwa kichwa. Udhaifu. Kichefuchefu. Kutapika. Kutokwa jasho. Kuchanganyikiwa. Manjano ya macho na ngozi. Mkojo kuwa rangi ya udhurungi.
Uingizaji hewa (hapana kama ni poda), mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga.
Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kuhara. Degedege. Kupoteza fahamu. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vilivyofunikwa; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: Xn, N
R: 22-40-50/53
S: (2-)-36/37-46-60-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 4.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 41S1334 (mango); 41GF1-II+III (mango); 41S2304 (myeyuko)
Msimbo wa NFPA: H 2; F 2; R 0;
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, vyakula na malisho. Hifadhi mahali pasipokuwa na unyevu au uchafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
NAPHTHALENE ICSC: 0667
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
MANGO NYEUPE KATIKA MAUMBO MBALIMBALI YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Inapowaka hutengeneza gesi zenye sumu na zinazowasha. Humenyuka pamoja na vioksidishaji vikali.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 10 ppm kama TWA; 15 ppm kama STEL; (ngozi); A4 (ACGIH 2005).
MAK: H Aina ya sarakani: 2; Aina inayoleta mabadiliko kwa seli za uzazi: 3B; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. Tazama Vidokezo.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii huweza kuathiri damukusababisha vidonda vya seli za damu (haemolysis). Tazama Vidokezo. Athari zinaweza kuchelewa. Mfiduo by ingestionhuweza kusababisha kifo. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri damu kusababisha upungufu wa chembechembe nyekundu za damu (chronic haemolytic anemia). Dutu hii huweza kuathiri jicho kusababisha mtoto wa jicho (development of cataract). Dutu hii ina uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 218°C
Sublimation slowly at room temperature
Kiwango myeyuko: 80°C
Uzito wiani: 1.16 g/cm³
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: hakuna
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 25°C: 11
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.42
Kiwango cha kumweka: 80°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 540°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 0.9-5.9
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 3.3
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kusababisha madhara yatakayoonekana baadaye katika mazingira ya maji.
VIDOKEZO
Baadhi ya watu wanaweza kuathiriwa zaidi na athari za nafthalini katika seli za damu
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005