| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizio wa maji, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 41°C.
|
Mfumo funge wa zaidi ya 41°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
|
|
| MFIDUO |
|
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kuumwa koo. Kupoteza fahamu.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Ngozi kavu. Wekundu. Maumivu.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Miwanivuli ya usalama.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni).
|
Ainisho ya EU Alama: Xi R: 10-37 S: (2-)-24/25 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 3 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 588 Msimbo wa NFPA: H 2; F 2; R 0; |
Isodhurika kwa moto iwapo ndani ya jengo. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali. Baridi.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI HATARI KWA MWILI: Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. HATARI ZA KIKEMIKALI: Humenyuka ikiwa na vioksidishaji vikali. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 25 ppm; 104 mg/m³ (kama TWA); 40 ppm; 167 mg/m³ (kama STEL) (ngozi) (ACGIH 1997). MAK: 25 ppm; 100 mg/m³; H (1996). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kupitia kwenye ngozi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Mfiduo husababisha kupungua fahamu. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Kioevu hukausha ngozi. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 132°C Kiwango myeyuko: -90°C Uzito wiani (maji = 1): 0.82 Umumunyifu katika maji: 2 g/100 ml Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.5 |
Kiwango cha kumweka: 41°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.0-5.5 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.43 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||