IODINE CYANIDE ICSC: 0662
Aprili 2005

Cyanogen iodide
CAS # 506-78-5 CNI
RTECS # NN1750000 Masi ya molekuli: 152.9
UN # 1588
EC # 006-007-00-5
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO

Utokeapo moto: poza mapipa n.k. kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji.
MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kuumwa koo. Kuumwa kichwa. Kuchanganyikiwa. Udhaifu. Kukosa pumzi. Degedege. Kupoteza fahamu. Tazama Vidokezo.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Huduma ya kusaidia kupumua ya mdomo kwa mdomo hairuhusiwi. Tumia oksijeni inayotolewa na wataalamu. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Maumivu. (Tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Mchomo. Kichefuchefu. Kutapika. Kuhara. (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Vaa glavu za kinga unapotoa utapishi. Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Huduma ya kusaidia kupumua ya mdomo kwa mdomo hairuhusiwi. Tumia oksijeni inayotolewa na wataalamu. Mpeleke kwa daktari. Tazama Vidokezo.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu. Uingizaji hewa. Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo vinavyokalafatika. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
Kisichoingiza hewa. Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: T+, N
R: 26/27/28-32-50/53
S: (1/2-)-7-28-29-45-60-61
Angalia: [A]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT5-I or 61GT5-I-Cy
Kinachotenganishwa na maunzi yasiokubaliana, vyakula na malisho. Kavu. Kilichofungwa vizuri. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri. Hifadhi mahali pasipokuwa na unyevu au uchafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
IODINE CYANIDE ICSC: 0662
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE NYEUPE YENYE HARUFU KALI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapogusana na asidi, besi, amonia alkoholi, na inapokanzwa kuzalisha gesi zenye sumu pamoja na sianidi hidrojeni. Humenyuka pamoja na dioksidi kaboni au polepole pamoja na maji kusababisha sianidi hidrojeni.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
Ikichanganyika katika hewa nyevu huunda mazingira ya sianidi ya hidrojeni:
TLV: (sianidi hidrojeni na baadhi ya chumvi za sianidi, kama CN) 4.7 ppm kama STEL; (kiwango cha juu); (ACGIH 2005).
MAK: (as CN) (kiwango cha kunuswa) 2 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: II (1); Kuingia kupitia kwa ngozi (H); Kundi la waja wazito lililo hatarini: C; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Kikolezo cha chembechembeya dhuru yaweza kufikiwa haraka ikitawanywa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera kwa ukali macho ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri ubadilishaji hewa wa seli kusababisha degedege na kupoteza fahamu. Mfiduo huweza kusababisha kifo. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Tazama Vidokezo.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri tezi thioridi.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: 146-147°C
Uzito wiani: 2.84 g/cm³
Umumunyifu katika maji: mmenyuko kwa upole
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 25.2°C: 130
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.54
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005