| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki lakini huongeza mwako wa dutu nyingine. Hutoa moshi wenye sumu sana ukiwa motoni. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka.
|
Usigusishe na dutu ziwakazo. Usigusishe na maji.
|
Moto unapotokea katika eneo: USITUMIE vitenzi vingine vyenye maji.
|
| MLIPUKO |
Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na maji au vitu za vikaboni.
|
|
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Mchomo. Kikohozi. Kuumwa koo. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Wekundu. Mibabuko nzito ya ngozi. Maumivu. Malengelenge.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana. Upofu wa kudumu.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
|
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Simamisha kutoka kwa gesi. Peleka silinda mahali salama pa wazi iwapo uvujaji hauwezi kuzuiliwa, na uwache itoke. KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo za kujikinga, zile ziwe ithinishwa kama inakinga kweli ClF_3 hata zile zinatamiwa kwa kupumua).
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho and combustible materials. Ainisho ya EU Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 2.3 Jasara tanzu za UN: 5.1 na 8 | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20G47 Msimbo wa NFPA: H 4; F 0; R 3; W,OX |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na dutu zenye kuungua na za kunakisi, vyakula na malisho. Baridi. Kavu.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: GESI OEVU ILIYOBANWA KARIBU ISO RANGI YENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Gesi hii ni nzito kuliko hewa. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana zaidi ya 220°C huzalisha gesi zenye sumu (misombo ya klorini na florini). Humenyuka kwa ukali ikiwa na maji, kioo. Humenyuka pamoja na aina yote ya plastiki, mpira na resini isipokuwa polima za florini. Maunzi yote yawakavyo huwaka yenyewe ikugusa dutu. Humenyuka kwa nguvu pamoja na dutu zinazoweza kuoksidiwa, metali na oksidi za metali. Inapasuka ikiguswa na maunzi kikaboni. Hutoa mvuke wenye sumu kali ikiguswa na asidi. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 0.1 ppm; 0.38 mg/m³ (viwango vya juu kabisa) (ACGIH 1997) |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Tazama Vidokezo. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 12°C Kiwango myeyuko: -76°C Umumunyifu katika maji: mmenyuko Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.18 |
|||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Chombo kilichokuwa na klorini triflorini lazima kisafishwe vizuri kabla ya kufunguliwa. Humenyuka kwa nguvu na vitenzi vya kuzimia moto kama vile maji. Kikomo thamani cha mfiduo matumizi ya kazi kisivukwe wakati wowote wa mfiduo amilifu. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Hakuna data za kutosha kuhusu athari za dutu hii kwa afya ya binadamu kwa hiyo kunahitajika uangalifu mkubwa. Usinyunyizie maji juu ya silinda inayovuja (kuzuia ulikaji wa silinda). Ona ICSC 0283 hydrogen fluoride.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||