DICYCLOHEXYL PHTHALATE ICSC: 0651
Aprili 1994

Phthalic acid, dicyclohexyl ester
1,2-Benzenedicarboxylic acid, dicyclohexylester
CAS # 84-61-7 C20H26O4 / C6H4(CO2C6H11)2
RTECS # TI0889000 Masi ya molekuli: 330.4
UN #
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka.
Usiwashe moto.
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi
Mtambo wa kutolea nje.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi
Glavu za kinga.
Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vilivyofunikwa; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru).
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Kinachotenganishwa na asidi, besi.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
DICYCLOHEXYL PHTHALATE ICSC: 0651
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
PODA FUWELE NYEUPE

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Humenyuka pamoja na asidi, besi.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru hautafikiwa au utafikiwa polepole sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C; wakati wa kunyunyiza au kutawanya, hata hivyo, kwa kasi zaidi.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri ini.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko ifikapo 0.5kPa: 222-228°C
Kiwango myeyuko: 66°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.4
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 150°C: 13.3
Kiwango cha kumweka: 207°C
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 3-4
DATA YA MAZINGIRA
Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira.
VIDOKEZO
Hakuna data za kutosha kuhusu athari za dutu hii kwa afya ya binadamu kwa hiyo kunahitajika uangalifu mkubwa.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005