COPPER (II) ORTHOARSENATE ICSC: 0648
Aprili 1993

Arsenic acid, copper salt
Copper arsenate
CAS # 10103-61-4 As2Cu3H8O12 / Cu3(AsO4)2• 4H2O
RTECS # None Masi ya molekuli: 540.5
UN # 1557
EC # 033-005-00-1
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kupumua kwa shida. Udhaifu. (Tazama Kumeza).
Mfumo funge na uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA!
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kuhara. Kutapika. Kuhisi hali ya kuungua kifuani na mdomoni.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Vuta kiombwe maunzi yaliyomwagika. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu).
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: T
R: 45-23/25
S: 53-45
Angalia: [A; E]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Kinachotenganishwa na asidi, vyakula na malisho. Baridi. Kilichofungwa vizuri. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
COPPER (II) ORTHOARSENATE ICSC: 0648
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
PODA BLUU AU BLUU-KIJANI

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu (arseniki ICSC 0013). Humenyuka pamoja na asidi kufanyiza gesi yenye sumu (arsini ICSC 0222).

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV (kama As): 0.2 mg/m³ (ACGIH 1993)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii na erosoli hii inakera macho na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva, njia ya utumbo, mpitio wa damu kusababisha kutokwa damu mno, kuishiwa maji na chumvi, mshtuko na kifo. Mfiduo wa kiwango cha chini huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa neva wa pembeni, ngozi, kiwamboute na ini kusababisha kugeuka kwa rangi ya asili, ugumu wa ngozi, vitobo vya tenganisho la pua, uvimbe wa neva (neuropathy), na kusababisha ini kuwa gumu (cirrhosis). Dutu hii husababisha kansa kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Umumunyifu katika maji: hakuna
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa maji. Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira.
VIDOKEZO
Jotoridi linalosababisha mtengano haijulikani katika maandiko. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005