DIACETONE ALCOHOL ICSC: 0647
Aprili 2005

4-Hydroxy-4-methylpentan-2-one
2-Pentanone, 4-hydroxy-4-methyl-
4-Hydroxy-2-keto-4-methylpentane
4-Hydroxy-4-methyl-2-pentanone
CAS # 123-42-2 C6H12O2 / (CH3)2C(OH)CH2COCH3
RTECS # SA9100000 Masi ya molekuli: 116.2
UN # 1148
EC # 603-016-00-1
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua. Tazama Vidokezo.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Mnyunyizio wa maji, povu linalokinza alkoholi, poda kavu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 58°C. (Tazama Vidokeso.)
Mfumo funge wa zaidi ya 58°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka. Tumia vifaa vya mkono visivyotoa cheche.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO


Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi Wekundu. Ngozi kavu. YAWEZA KUFYONZWA!
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoa vyanzo vyote vya moto. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni. Funika dutu iliyomwagika kwa kifyonzi ajizi. Kusanya salio kwa uangalifu.
Ainisho ya EU
Alama: Xi
R: 36
S: (2-)-24/25
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30GF1-III
Msimbo wa NFPA: H 1; F 2; R 0;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na asidi, besi, amini na vioksidishaji.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
DIACETONE ALCOHOL ICSC: 0647
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa au inapochomwa au inapogusana na asidi, besi na amini, huzalisha asetoni, mesityl alcohol. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji kutoa gesi inayoweza kuwaka/kulipuka (hidrojeni - tazama ICSC 0001)

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 50 ppm kama TWA; (ACGIH 2005).
MAK: 20 ppm, 96 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: I(2); kuingia kupitia kwa ngozi (H); Kundi la waja wazito lililo hatarini: IIc; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Mchanganyiko unaoweza kudhuru yaweza kutokea haiwezi au yaweza kufikia kwa upolekama dutu hii inavukiza kwa hewa yenye joto ya 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kumeza kioevu hiki kunaweza kusababisha madhara kwenye mapafu kukifyonza na kunaweza kuleta kichomi kinachotokana na kemikali. Mfiduo juu ya OEL huweza kuleta kupungua kwa fahamu.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Kioevu hukausha ngozi.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 169-171°C
Kiwango myeyuko: -47°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.93
Umumunyifu katika maji: kuchanganyika
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 0.108
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.0
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.0048
Kiwango cha kumweka: 58°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 640°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.8-6.9
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -0.14 to 1.03 (imekadiriwa)
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Bidhaa ya kiufundi inaweza kuwa na hadi 5% ya asetoni (tazama ICSC0087) kusababisha kuwa na kiwango cha juu cha kuweza kuwaka. UN huainisha dutu kiteknikali kama 3 (ainisho ya UN ya hatari), II (kikundi ufungashaji cha UN).
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005