BROMOCHLORODIFLUOROMETHANE ICSC: 0635
Oktoba 1997

Freon 12 B 1
R 12 B 1
Halon 1211
(silinda)
CAS # 353-59-3 CBrClF2
RTECS # PA5270000 Masi ya molekuli: 165.4
UN # 1974
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Ukanzaji unaweza kusababisha ongezeko la kanieneo na kuleta athari ya kupasuka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO

Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO


Kuvuta pumzi Kusinzia. Kupoteza fahamu.
Uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
Glavu za kuhami baridi.
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Mpeleke kwa matibabu.
Macho INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
Kingao cha uso.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza


KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Uingizaji hewa. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 2.2

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20G39
Isodhurika kwa moto iwapo ndani ya jengo.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
BROMOCHLORODIFLUOROMETHANE ICSC: 0635
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
GESI OEVU, ILIYOBANWA, YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Gesi hii ni nzito kuliko hewa na huweza kujilimbikiza katika eneo ambalo dari liko chinichini na kusababisha upungufu wa oksijeni.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapogusana na miali ya moto au nyuso zenye joto sana, huzalisha gesi zenye sumu kama vile fosjini, floridi hidrojeni, kloridi hidrojeni, bromidi hidrojeni.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Kisipodhibitiwa kioevu hiki huvukiza haraka sana na kusababisha ukifishwaji mno wa hewa na kuleta hatari kubwa ya kukosekana hewa katika maeneo funge.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Uvukizaji wa haraka wa kioevu huweza kusababisha jamidi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa moyo na mishipa, kusababisha ugonjwa wa moyo.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: -4°C
Kiwango myeyuko: -160.5°C
Umumunyifu katika maji: hakuna
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 5.7
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.1
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa tabaka ya ozoni.
VIDOKEZO
Ukolezi mkubwa katika hewa husababisha unakisi wa oksijeni pamoja na hatari ya kupoteza fahamu au kufa. Pima kiasi cha oksijeni kabla ya kuingia katika eneo. Usitumie karibu na moto au uso moto, au wakati wa kulehemu.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005