| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua sana. Tazama Vidokezo. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na dutu ziwakazo. Usigusishe na hewa. Usigusishe na nyuso za moto. Usigusishe na vioksidishaji, halojeni, sulfuri na besi kali.
|
Mnyunyizio wa maji, mchanga ulioloa.
|
| MLIPUKO |
|
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU! EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Mchomo. Kikohozi. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi. Kuumwa koo. Kupoteza fahamu. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Wekundu. Mibabuko ya ngozi. Maumivu. Malengelenge.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena. Mpeleke kwa matibabu. Vaa glavu za kinga unapotoa huduma ya kwanza. See Notes.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Upofu. Kuungua kunakopenya sana.
|
Miwanivuli ya usalama, Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Maumivu ya tumbo. Mchomo. Mshtuko au kuzimia. Kupoteza fahamu.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Kupumzika. Vaa glavu za kinga unapotoa utapishi. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Funika dutu iliyomwagika kwa mchanga ulioloa au tope. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi kisha peleka mahala pa usalama. Usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu.
|
Kisichoingiza hewa. Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Alama: F, T+, C, N R: 17-26/28-35-50 S: (1/2-)-5-26-38-45-61 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 4.2 Jasara tanzu za UN: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: I | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 42S1381-w Msimbo wa NFPA: H 3; F 3; R 1; |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, vyakula na malisho. Weka chini ya maji.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: MANGO FUWELE ANGAVU, INAYOONEKANA KAMA NTA NYEUPE HADI MANJANO. HUGEUKA GIZA INAPOFIDULIWA NA MWANGA. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii huweza kuwaka papo hapo inapogusana na hewa kuzalisha mafusho yenye sumu (oksidi za fosforasi). Humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji, halojeni na sulfuri, kusababisha athari ya moto na mlipuko. Humenyuka besi kali kusababisha gesi yenye sumu (fosfini). VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 0.02 ppm kama TWA; (ACGIH 2003). MAK: 0.1 mg/m³ (kiwango cha kunuswa); Aina ya kiwango cha juu: I(1); Kundi la waja wazito lililo hatarini: D; (DFG 2003). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa. Kuvuta pumzi ya mvuke wake kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Dutu hii huweza kuathiri mafigo, ini. Mfiduo huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Dutu hii huweza kuathiri mifupa. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Hutengana chini ya kiwango myeyuko ifikapo 44°C Uzito wiani: 1.83 g/cm³ Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 0.0003 Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 3.5 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.42 |
Kiwango cha kumweka: < 20°C Jotoridi la kujiwasha: 30°C | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Inaweza kujiwasha yenyewe baada ya moto kuzimwa. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||