METHYL ACRYLATE ICSC: 0625
Novemba 2003

Acrylic acid, methyl ester
Methyl-2-propenoate
2-Propenoic acid, methyl ester
CAS # 96-33-3 C4H6O2 / CH2=CHCOOCH3
RTECS # AT2800000 Masi ya molekuli: 86.1
UN # 1919
EC # 607-034-00-0
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua sana.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, AFFF, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kukosa pumzi. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kuhara. Kichefuchefu. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoa vyanzo vyote vya moto. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vyenye mifuniko. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni. Vazi linalokinga kemikali.
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa.
Ainisho ya EU
Alama: F, Xn
R: 11-20/21/22-36/37/38-43
S: (2-)-9-25-26-33-36/37-43
Angalia: [D]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30S1919
Msimbo wa NFPA: H 3; F 3; R 2;
Isodhurika kwa moto. Tazama Hatari za Kikemikali. Kilichopozwa. Weka gizani. Kilichofungwa vizuri. Hifadhi iwapo tu imetulia.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
METHYL ACRYLATE ICSC: 0625
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU KALI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. Mvuke haina kuzuisi na yaweza kuwa polima katika matundu au vizimio vya miali ya moto vya matangi na yaweza kuziba tundu.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii huweza kupolimisha mara moja yenyewe kutokana na kupata joto kwa kuathiriwa na mwanga na inapogusana na peroksidi. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na asidi kali, besi kali, vioksidishaji vikali kusababisha athari ya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 2 ppm kama TWA; (ngozi); A4; (ACGIH 2003).
MAK: 5 ppm, 18 mg/m³; Sh; Aina ya kiwango cha juu: I(1); Kundi la waja wazito lililo hatarini: IIc; (DFG 2003).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera ngozi na njia ya upumuaji, na inakera kwa ukali macho.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 80.5°C
Kiwango myeyuko: -76.5°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.95
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 6
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 9.1
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.0
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.18
Kiwango cha kumweka: -2.8°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 468°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 2.8-25
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.8
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Ongezeko la kiimarishaji au kiviza huweza kuathiri tabia ya kitoksini za dutu hii, shauriana na mtaalam. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005