DIETHANOLAMINE ICSC: 0618
Oktoba 2002

2,2'-Iminodiethanol
DEA
2,2'-Dihydroxydiethylamine
CAS # 111-42-2 C4H11NO2 / (CH2CH2OH)2NH
RTECS # KL2975000 Masi ya molekuli: 105.2
UN #
EC # 603-071-00-1
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka.
Usiwashe moto.
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!

Kuvuta pumzi
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Mchomo.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari. Kupumzika.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio A/P2 cha mvuke kikaboni na vumbi linalodhuru).
Ainisho ya EU
Alama: Xn
R: 22-38-41-48/22
S: (2-)-26-36/37/39-46
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Msimbo wa NFPA: H 1; F 1; R 0;
Kinachotenganishwa na asidi, na vioksidishaji vikali. Kavu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
DIETHANOLAMINE ICSC: 0618
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE NYEUPE AU KIOEVU KIRISHAI KISICHO RANGI KINATACHO CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu. Mmumunyo huu katika maji ni besi kali ya kati. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji vikali, asidi kali. Hushambulia shaba, zinki, alumini, na aloi zake.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 2 mg/m³; (ngozi); (ACGIH 2002).
Ainisho ya MAK: Sh, H; Aina ya sarakani: 3A; (2002)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru hautafikiwa au utafikiwa polepole sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri ini na mafigo.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 269°C
Kiwango myeyuko: 28°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.09 (kioevu)
Umumunyifu katika maji: vizuri sana
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: <1
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.65
Kiwango cha kumweka: 134°C o.c.
Jotoridi la kujiwasha: 662°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.7-9.8
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -1.43
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Usichukue nguo za kazi nyumbani.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005