BARIUM CHLORATE ICSC: 0613
Oktoba 2000

Chloric acid, barium salt
CAS # 13477-00-4 BaCl2O6 / Ba(ClO3)2
RTECS # FN9770000 Masi ya molekuli: 304.2
UN # 1445
EC # 017-003-00-8
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki lakini huongeza mwako wa dutu nyingine. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka.
Usigusishe na dutu ziwakazo. Usigusishe na dutu za kikaboni, poda za metali, chumvi za amonia na kinakisishaji.
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na: tazama Hatari za Kikemikali.
USIACHE kikaathiriwa na msuguano au mshtuko. Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo. (Tazama Kumeza).
Uingizaji hewa (hapana kama ni poda), mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu.
Glavu za kinga.
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Ngozi kugeuka kuwa bluu. Kuchanganyikiwa. Degedege. Kuhara. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kupoteza fahamu. Kutapika. Udhaifu.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Shauriana na mtaalam endapo mwagiko ni mkubwa. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Osha salio kwa maji mengi. Usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: O, Xn
R: 9-20/22
S: (2-)-13-27
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 5.1
Jasara tanzu za UN: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 812
Msimbo wa NFPA : H 2; F 0; R 1; ox
Kinachotenganishwa na dutu zenye kuungua na za kunakisi, dutu zenye amonia, poda za metali, vyakula na malisho.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
BARIUM CHLORATE ICSC: 0613
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
PODA FUWELE ISO RANGI

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Misombo isiyohimili mshtuko hutengenezwa kwa dutu za kikaboni, kinakisishaji, dutu zenye amonia na poda za metali. Dutu hii hutengana kwa ukali sana inapokanzwa huzalisha oksijeni na mafusho yenye sumu, kusababisha athari ya moto na mlipuko. Dutu hii ni kioksidishaji madhubuti na humenyuka iwapo na maunzi yanayoweza kuwaka na yanayonakisi.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV (kama Ba): 0.5 mg/m³ (kama TWA) A4 (ACGIH 1999).
0.5 mg/m³ EC OELs
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa hasa iwapo katika hali ya poda.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri damu na mfumo wa neva, kusababisha kufanyika kwa methemoglobini. Mfiduo huweza kusababisha upungufu wa potasiamu (hypokalemia), kusababisha ugonjwa wa moyo na mvurugano wa misuli. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Mfiduo huweza kusababisha kifo.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Hutengana kabla ya kuyeyuka: 250°C
Uzito wiani: 3.2 g/cm³
Umumunyifu katika maji, g/100 ml: 27.4 (vizuri)
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Dalili za paralysis hazijitokezi mpaka masaa kadhaa yamepita. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi. CAS 10294-38-9 ni nambari ya Bariamu klorati, monohidrati. Haitahimili mshtuko ikiingiwa na: tazama Hatari za Kikemikali.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005