XENON ICSC: 0609
Oktoba 1997

(silinda)
CAS # 7440-63-3 Xe
RTECS # ZE1280000 Masi ya atomi: 131.3
UN # 2036
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Ukanzaji unaweza kusababisha ongezeko la kanieneo na kuleta athari ya kupasuka.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO

Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO


Kuvuta pumzi Msongo wa hewa (asfiksianti sahili).
Uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
Glavu za kuhami baridi. Mavazi ya kinga.
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Mpeleke kwa matibabu.
Macho INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
Miwanivuli ya usalama, kingao cha uso.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza


KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Uingizaji hewa. (Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 2.2

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20G30
Isodhurika kwa moto iwapo ndani ya jengo.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
XENON ICSC: 0609
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
GESI ISO RANGI, ISO HARUFU, OEVU

HATARI KWA MWILI:
Gesi hii ni nzito kuliko hewa na huweza kujilimbikiza katika eneo ambalo dari liko chinichini na kusababisha upungufu wa oksijeni.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Kisipodhibitiwa kioevu hiki huvukiza haraka sana na kusababisha ukifishwaji mno wa hewa na kuleta hatari kubwa ya kukosekana hewa katika maeneo funge.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Kioevu hiki huweza kusababisha jamidi.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: -108°C
Kiwango myeyuko: -112°C
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 108
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 3300
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.54
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.4
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Ukolezi mkubwa katika hewa husababisha unakisi wa oksijeni pamoja na hatari ya kupoteza fahamu au kufa. Pima kiasi cha oksijeni kabla ya kuingia katika eneo. Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu. Nambari nyingine za UN: 2591, xenon, refridgerated liquid, ainisho ya UN ya hatari 2.2.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005