ZINC PHOSPHIDE ICSC: 0602
Machi 2001

Trizinc diphosphide
CAS # 1314-84-7 Zn3P2
RTECS # ZH4900000 Masi ya molekuli: 258.1
UN # 1714
EC # 015-006-00-9
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki lakini hutengeneza gesi inayoungua ikigusana na maji au hewa nyevunyevu.
Usigusishe na asidi, maji au vioksidishaji.
Moto unapotokea katika eneo: poda. USITUMIE maji, USITUMIE dioksidi kaboni.
MLIPUKO

Utokeapo moto: poza mapipa n.k. kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji.
MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kutokwa jasho. Uchovu. Kichefuchefu. Kuhara. Kutapika.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Mchomo.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Maumivu. Kuogopa mwanga.
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kichefuchefu. Kutotembea vizuri. Uchovu. Kutapika. Kikohozi. Kuhara. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kupumua kwa shida. Kupoteza fahamu.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Tazama Vidokezo. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vikavu; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu.
Ainisho ya EU
Alama: F, T+
R: 15/29-28-32
S: (1/2-)-3/9/14-30-36/37-45
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 4.3
Jasara tanzu za UN: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 43G15
Msimbo wa NFPA : H 3; F 3; R 1;
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi, maji. Kavu. Baridi. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ZINC PHOSPHIDE ICSC: 0602
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE, LAHAMU AU PODA KIJIVU ILIYOKOZA, YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa na inapogusana na asidi, na taratibu pamoja na maji huzalisha mafusho yenye sumu na iwakayo ya oksidi za fosforasi na oksidi zinki, na fosfini. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji vikali kusababisha athari ya moto.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka hasa iwapo katika hali ya poda.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri ini, mafigo, moyo na mfumo wa neva. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kuleta kifo. Kuvuta pumzi fosfini hutokana na fosfidi zinki kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo).

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa neva.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 1100°C
Kiwango myeyuko: 420°C
Uzito wiani: 4.6 g/cm³
Umumunyifu katika maji: hakuna, taratibu hutengana
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa ndege na mamalia.
VIDOKEZO
Humenyuka kwa nguvu na vitenzi vya kuzimia moto kama vile maji na dioksidi kaboni. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya mnyunyuzio mwafaka unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Iwapo mgonjwa atatapishwa baada ya kumeza, kusanya matapishi katika mfuko wa plastiki ili kuzuia kutoka kwa fosfini. Blue-ox, Gopha-rid, Kilrat, Mous-Con, Phosvin, Ratol, Rumetan na Zinc-Tox ni majina ya kibiashara. Pia shauriana na ICSC 0694 Phosphine.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005