| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka.
|
Usiwashe moto.
|
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizo wa maji, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
|
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.
|
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa.
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! Mchomo. Wekundu. Mibabuko ya ngozi.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
|
Miwanivuli ya usalama, kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Mchomo. Maumivu ya tumbo. Kichefuchefu. Kutapika. Kuhara. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Mshtuko au kuzimia.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Kupumzika. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoa vyanzo vyote vya moto. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo vinavyokalafatika. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia).
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari. Ainisho ya EU Alama: T, N R: 24/25-34-51/53 S: (1/2-)-26-36/37/39-45-61 Angalia: [C] Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 672
|
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho, anhidridi za asidi, kloridi za asidi, besi na vioksidishaji.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU AU FUWELE NYEUPE HADI MANJANO, YENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa. HATARI ZA KIKEMIKALI: Humenyuka pamoja na anhidridi asidi, kloridi asidi, besi na vioksidishaji. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho na ngozi. Husababisha ubabuzi inapomezwa. Dutu hii inakera njia ya upumuaji. Tazama Vidokezo. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Tazama Vidokezo. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 203-225°C Kiwango myeyuko: 25-75°C Uzito wiani: 1.02-1.13 g/cm³ Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: 4-8 Kanieneo mvuke, Pa ifikapo °C: 0.5-37 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.2 |
Kiwango cha kumweka: 61-95°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 599°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.4-? Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.23-2.36 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Hakuna data za kutosha kuhusu athari za dutu hii kwa afya ya binadamu, kwa hiyo unahitajika uangalifu mkubwa. Health effects may be similar to those of phenol and related compounds. Pia shauriana na ICSC 0070 (Phenol). Mapendekezo kwenye kadi hii pia yanahusu 3,4-xylenol (CAS 95-65-8), 2,5-xylenol (CAS 95-87-4), 2,4-xylenol (CAS 105-67-9), 2,3-xylenol (CAS 526-75-0) na 2,6-xylenol (CAS 576-26-1).
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||