| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
|
|
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kuumwa koo. Kizunguzungu. Kuchanganyikiwa.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Wekundu. INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
|
Glavu za kuhami baridi.
|
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
|
Ainisho ya EU Alama: F+, T R: 45-12 S: 53-45 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 2.1 | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Msimbo wa NFPA: H 2; F 0; R 1; Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20G2F-9 |
Isodhurika kwa moto. Baridi. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri. Kinachotenganishwa na vioksidishaji. Hifadhi iwapo tu imetulia.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: GESI OEVU ILIYOBANWA YENYE HARUFU KALI. HATARI KWA MWILI: Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa. HATARI ZA KIKEMIKALI: Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji. Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha gesi zenye sumu. Dutu hii hupolimisha kwa kuathiriwa na joto au mwanga. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: kama TWA 0.5 ppm A2 (ACGIH 2001). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Uvukizaji wa haraka wa kioevu huweza kusababisha jamidi. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Dutu hii huenda inasababisha kansa kwa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 15.6°C Kiwango myeyuko: -139.5°C Uzito wiani (maji = 1): 1.49 Umumunyifu katika maji: hakuna Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 119 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.7 |
Kiwango cha kumweka: gesi iunguayo Jotoridi la kujiwasha: 530°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 9-15 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.57 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Ongezeko la kiimarishaji au kiviza huweza kuathiri tabia ya kitoksini za dutu hii, shauriana na mtaalam. Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||