| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua sana. Ukanzaji unaweza kusababisha ongezeko la kanieneo na kuleta athari ya kupasuka.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Poda, AFFF, povu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza). USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
|
| MFIDUO |
|
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kuchanganyikiwa. Kikohozi. Kizunguzungu. Kusinzia. Mazimbwezimbwe. Kuumwa kichwa. Kuumwa koo.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Wekundu.
|
Glavu za kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Miwani ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Ainisho ya EU Alama: F R: 11 S: (2-)-9-16-29-33 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 3 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 120 Msimbo wa NFPA: H 2; F 3; R 0; |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali. Baridi. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. Kutokana na mtiririko, mchukucho n.k., chaji za kiumemetuamo huweza kutokea. HATARI ZA KIKEMIKALI: Humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki. MAK haijathibitishwa. |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kusababisha kupoteza fahamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 101°C Kiwango myeyuko: -93°C Uzito wiani (maji = 1): 0.7 Umumunyifu katika maji: hakuna Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 38°C: 10 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.9 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.3 Kiwango cha kumweka: -5°C Jotoridi la kujiwasha: 391°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 0.8-4.8 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 4.55 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini. Kuzidisha kwa kemikali yaweza kutokea kwa samaki. Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Madhara ya afya yatokanayo na kuingia mwilini dutu hii hayajachunguzwa.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||