| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua mno. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
USITUMIE maji. AFFF, poda, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua.
|
Utokeapo moto: poza mapipa n.k. kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji.
|
| MFIDUO |
|
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kuumwa koo. Mchomo. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu. Tazama Vidokezo.
|
| Ngozi |
Wekundu. Maumivu. Malengelenge. Mibabuko ya ngozi.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Mchomo. Maumivu ya tumbo. Mshtuko au kuzimia.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Usimpe chochote cha kunywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Usitumie vyombo vya plastiki. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga mkavu au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia).
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Alama: F+, C R: 12-14-17-20/22-29-35 S: (2-)-7/9-16-26-36/37/39-43-45 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 4.3 Jasara tanzu za UN: 3 na 8 Kikundi Ufungashaji cha UN: I | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 43S1295 Msimbo wa NFPA: H 3; F 4; R 2; W |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho na maunzi yasiokubaliana. Tazama Hatari za Kikemikali. Baridi. Kavu. Kilichofungwa vizuri. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI, VUKIVU, KIFUKACHO CHENYE HARUFU KALI. HATARI KWA MWILI: Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho babuzi na yenye sumu kama vile kloridi hidrojeni. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na maji, vioksidishaji vikali, asidi kali, besi kusababisha kloridi hidrojeni (tazama ICSC 0163). Hushambulia metali nyingi iwapo kuna maji. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki. |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa. Kuvuta pumzi ya mvuke wake kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Kuvuta pumzi kunaweza kusababisha pumu (tazama Vidokezo). Mfiduo huweza kusababisha kifo. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Tazama Vidokezo. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 31.8°C Kiwango myeyuko: -126.5°C Uzito wiani (maji = 1): 1.34 Umumunyifu katika maji: mmenyuko Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 65.8 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.7 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 3.3 Kiwango cha kumweka: -27°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 185°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.2-90.5 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Humenyuka kwa nguvu na vitenzi vya kuzimia moto kama vile maji. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Asili ya taaluma ya sumu ni kama methilidiklorosilini (ICSC0297).
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||