| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
|
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
|
| MLIPUKO |
|
|
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Kuumwa koo. Kikohozi. Mchomo. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kutapika. Kukosa pumzi. Kupumua kwa shida. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Uingizaji hewa (hapana kama ni poda), mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Maumivu. Wekundu. Malengelenge. Mibabuko ya ngozi.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Maumivu. Wekundu. Kuungua kunakopenya sana.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Mchomo. Maumivu ya tumbo. Mshtuko au kuzimia.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Kupumzika. Mpeleke kwa daktari. Tazama Vidokezo.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo imejazwa maji; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Katisha salio kwa uangalifu kutumia alkali kama vile magadi (bikabonati sodiamu, hidroksidi sodiamu). Kisha osha kwa maji mengi. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Ainisho ya EU Alama: C R: 35 S: (1/2-)-24/25-26-45 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 8 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 80G09
|
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Tazama Hatari za Kikemikali. Baridi. Kavu. Kilichofungwa vizuri. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: FUWELE ISO RANGI NA RISHAI YENYE HARUFU KALI. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi kama vile kloridi hidrojeni na klorofomi (chloroform). Mmumunyo katika maji ni asidi kali humenyuka vikali ikiwa na besi na husababisha ulikaji kwa metali nyingi. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 1 ppm; 6.7 mg/m³ (kama TWA) A4 (ACGIH 1998) |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa. Kuvuta pumzi ya mvuke wake kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 198°C Kiwango myeyuko: 58°C Uzito wiani: 1.6 g/cm³ Umumunyifu katika maji: vizuri sana Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 51°C: 133 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 5.6 |
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.7 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||