| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka.
|
Usiwashe moto.
|
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
|
| MLIPUKO |
|
|
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)! EPUKA MFIDUO KWA VIJANA NA WATOTO!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Kutokwa jasho. Kichefuchefu. Kutapika. Kizunguzungu. Msongo/mfinyo (wa jicho), kukakamaa kwa msuli, utokaji mate kwa wingi. Kupumua kwa shida. Degedege. Kupoteza fahamu. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! (Tazama Kuvuta pumzi).
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Pupillary constriction. Kiwaa.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Kichefuchefu. Kutapika. Udhaifu. Msokoto wa tumbo. Kuhara. Msongo/mfinyo (wa jicho), kukakamaa kwa msuli, utokaji mate kwa wingi. Kupumua kwa shida. Kupoteza fahamu.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio A/P2 cha mvuke kikaboni na vumbi linalodhuru).
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari. Ainisho ya EU Alama: Xn R: 22-43 S: (2-)-24-37 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G41c
|
Kinachotenganishwa na besi kali, vyakula na malisho. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: FUWELE NYEUPE HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa na inapogusana na asidi na besi huzalisha mafusho yenye sumu. Hushambulia metals nyingi. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka ikifanyiza vumbi. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva kwa kuzuia kolinesterasi, kusababisha degedege, kutoweza kupumua na kifo. Kizuizi cha kolinesterasi. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa neva, kusababisha upungufu mkubwa wa kolinesterasi ya damu. Kizuizi cha kolinesterasi; uwezekano wa madhara yake kulimbikizana: tazama athari za papo hapo/dalili. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango myeyuko: 83-84°C Uzito wiani (maji = 1): 1.73 Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: 15.4 Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: <0.01 |
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.48 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa nyuki na samaki.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Dalili za madhara ya sumu ya papo hapo hazijitokezi mpaka masaa kadhaa yamepita. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Mapendekezo yaliyopo kwenye kadi hii yanahusu dutu halisi. Mara nyingi mazao yaliyoundwa kibiashara ni michanganyiko inayojumuisha pamoja na vitu vingine, vimumunyishaji au vitenzi vingine vinarekebisha tabia na sumu, maumbile na tabia za kikemikali. Acrol, DEP, DANEX, DIMETOX ni majina ya kibiashara.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||