TETRAHYDROFURAN ICSC: 0578
Oktoba 1997

Tetramethylene oxide
Diethylene oxide
1,4-Epoxybutane
Oxacyclopentane
CAS # 109-99-9 C4H8O / (CH2)3CH2O
RTECS # LU5950000 Masi ya molekuli: 72.1
UN # 2056
EC # 603-025-00-0
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua sana.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, povu linalokinza alkoholi, maji mengi, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kuumwa koo. Kupoteza fahamu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Ngozi kavu. Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni).
Kisichoingiza hewa.
Ainisho ya EU
Alama: F, Xi
R: 11-19-36/37
S: (2-)-16-29-33
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 601
Msimbo wa NFPA: H 2; F 3; R 1;
Isodhurika kwa moto. Tazama Hatari za Kikemikali. Hifadhi iwapo tu imetulia.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
TETRAHYDROFURAN ICSC: 0578
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii huweza kutengeneza peroksidi lipukaji. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji vikali, besi kali na baadhi ya halidi za metali kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia aina fulani za plastiki, mpira na mipako.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV (kama TWA): 200 ppm; 590 mg/m³
(kama STEL): 250 ppm; 737 mg/m³ (ACGIH 1997)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii au mvuke huu inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri ubongo kwa hali ya juu kusababisha uzingisi (narcosis).

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 66°C
Kiwango myeyuko: -108.5°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.89
Umumunyifu katika maji: kuchanganyika
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 19.3
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.5
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.28
Kiwango cha kumweka: -14.5°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 321°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 2-11.8
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
p-Kresol au haidroqwinoni huwa zinatumiwa kama vidhibiti. Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru. Ongezeko la kiimarishaji au kiviza huweza kuathiri tabia ya kitoksini za dutu hii, shauriana na mtaalam. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Kagua kama kuna peroksidi kabla ya kunereka; iwapo chanya fanya iwe salama.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005