| |||||||||||
| |||||||||||
|
|||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka.
|
Usiwashe moto.
|
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
|
|
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kukosa pumzi.
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Mchomo.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Kuchanganyikiwa. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kutapika. Udhaifu. Mshtuko au kuzimia.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Mpeleke kwa daktari. Usimtapishe.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vyenye mifuniko. Vaa kingao cha uso kinachofaa. Kinga ya ziada ya binafsi: nguo za kukinga mwili wote na kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Alama: T R: 45 S: 53-45 Angalia: [H, J, M] Ainisho ya UN | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Msimbo wa NFPA: H 2; F 2; R 0;
|
Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU NYEUSI HADI KAHAWIA, KAMA MAFUTA CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI ZA KIKEMIKALI: Inapowaka hutengeneza mafusho yenye sumu. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki. |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C na hasa wakati wa kunyunyiza. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuchomwa na jua kunaweza kuzidisha athari ya kuwashwa inayosababishwa na kresoti katika ngozi na macho na kusababisha kuungua. Mfiduo kwa kumeza huweza kuleta kifo. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Ikigusa ngozi mara kwa mara au kwa muda mrefu kinaweza kusababisha ugonjwa wa ngozi na kuzidi kuongezeka kwa rangi ya asili ya ngozi. Dutu hii huenda inasababisha kansa kwa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 200-400°C Kiwango myeyuko: takribani 20°C Uzito wiani: 1.0-1.17 g/cm³ Umumunyifu katika maji: ni dhaifu Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: takribani 6 |
Kiwango cha kumweka: zaidi ya 66°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 335°C | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa kuchafua mchanga, maji ya ardhini. Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||