SODIUM ALUMINATE ICSC: 0566
Aprili 2000

Aluminium sodium oxide
Sodium aluminium dioxide
CAS # 1302-42-7 NaAlO2
RTECS # BD1600000 Masi ya molekuli: 82
UN # 2812
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Mchomo. Kuumwa koo. Kikohozi. Kupumua kwa shida.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu. Malengelenge.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kiwaa. Kuungua kunakopenya sana.
Miwanivuli ya usalama, kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Mchomo. Mshtuko au kuzimia.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Osha salio kwa maji mengi. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 8
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 80G09
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho, asidi. Kavu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
SODIUM ALUMINATE ICSC: 0566
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
PODA NYEUPE, RISHAI

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Mmumunyo huu katika maji ni besi kali, humenyuka vikali ikiwa na asidi na husabisha ulikaji hadi alumini, bati na zinki. Humenyuka pamoja na chumvi za amonia kusababisha athari ya moto.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV (kama Al chumvi mmumunyifu): 2 mg/m³; (kama TWA) (ACGIH 1999)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: 1650°C
Uzito wiani: >1.5 g/cm³
Umumunyifu katika maji: vizuri sana
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Namba nyingine za UN: 1819 (sodium aluminate, mmumunyo 80%): ainisho ya hatari: 8, kikundi ufungashaji ya UN: III. Namba nyingine ya CAS: 11138-49-1.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005