PROPYLENE ICSC: 0559
Novemba 1998

Methylethylene
Propene
Methylethene
(silinda)
CAS # 115-07-1 C3H6 / CH2CHCH3
RTECS # UC6740000 Masi ya molekuli: 42.1
UN # 1077
EC # 601-011-00-9
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua mno.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Funga ugavi; kama haiwezekani na hakuna hatari kwa mazingira, acha moto uwake hadi ujizime; ama sivyo zima kwa kutumia poda, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya gesi/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza) ikiwa ni kioevu.
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO


Kuvuta pumzi Kusinzia. Msongo wa hewa (tazama Vidokezo).
Uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
Glavu za kuhami baridi.
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Tazama Ngozi.
Miwanivuli ya usalama, kingao cha uso.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.

KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
Ainisho ya EU
Alama: F+
R: 12
S: (2-)-9-16-33
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 2.1

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 137.
Msimbo wa NFPA: H 1; F 4; R 1;
Isodhurika kwa moto. Baridi.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
PROPYLENE ICSC: 0559
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
GESI OEVU ILIYOBANWA ISO RANGI

HATARI KWA MWILI:
Gesi hii ni nzito kuliko hewa. na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana na huweza kujilimbikiza katika eneo ambalo dari liko chinichini na kusababisha upungufu wa oksijeni. Kutokana na mtiririko, mchukucho n.k., chaji za kiumemetuamo huweza kutokea.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Humenyuka vikali ikiwa na vioksidishaji kusababisha athari ya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Isipodhibitiwa gesi hii huweza kusababisha kukosekana hewa kwa kupunguza kiasi cha oksijeni hewani katika maeneo funge.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Uvukizaji wa haraka wa kioevu huweza kusababisha jamidi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Mfiduo husababisha kupungua fahamu. Tazama Vidokezo.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: -48°C
Kiwango myeyuko: -185°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.5
Umumunyifu katika maji: mbaya
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 25°C: 1158
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.5
Kiwango cha kumweka: gesi iunguayo
Jotoridi la kujiwasha: 460°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 2.4-10.3
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.77
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Ukolezi mkubwa katika hewa husababisha unakisi wa oksijeni pamoja na hatari ya kupoteza fahamu au kufa. Pima kiasi cha oksijeni kabla ya kuingia katika eneo. Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005