| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua sana. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na vioksidishaji.
|
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizo wa maji, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kuyumbayumba. Kuchanganyikiwa. Kizunguzungu. Kusinzia. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Udhaifu.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko.
|
| Ngozi |
Ngozi kavu.
|
Glavu za kinga.
|
Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kiwaa.
|
Miwanivuli ya usalama.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Maumivu ya tumbo. Kuumwa koo. Kutapika. (Tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama.
|
Ainisho ya EU Alama: F, Xi R: 11-41-67 S: (2-)-7-16-24-26-39 Angalia: [C] Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 3 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 543 Msimbo wa NFPA : H 1; F 3; R 0; |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali. Baridi. Kilichofungwa vizuri. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI, ANGAVU, CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Mvuke huu huchanganyika vema na hewa, mchanganyiko unaolipuka hutokea kwa urahisi. HATARI ZA KIKEMIKALI: Humenyuka pamoja na vioksidishaji kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia aina fulani za plastiki na mpira. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 200 ppm (kama TWA) (ngozi) (ACGIH 1999). TLV (kama STEL): 250 ppm (ngozi) (ACGIH 1999). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C wakati wa kunyunyiza au kutawanya, hata hivyo, kwa kasi zaidi. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kuleta kuzirai, kupoteza fahamu. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Kioevu hukausha ngozi. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 97°C Kiwango myeyuko: -127°C Uzito wiani (maji = 1): 0.8 Umumunyifu katika maji: kuchanganyika Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 2.0 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.1 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.02 Kiwango cha kumweka: 15°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 371°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 2.1-13.5 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.25 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||