| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki lakini huongeza mwako wa dutu nyingine. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usigusishe na maji na vinavyoweza kuwaka.
|
Poda, dioksidi kaboni, mchanga mkavu, USITUMIE vitenzi vya majimaji.
|
| MLIPUKO |
|
|
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Mchomo. Kikohozi. Kukosa pumzi. Kuumwa koo. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Mibabuko ya ngozi. Maumivu. Malengelenge.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu. Vaa glavu za kinga unapotoa huduma ya kwanza.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Msokoto wa tumbo. Mchomo. Kuhara. Kuumwa koo. Kutapika.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Usimtapishe. Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo. Katisha salio kwa uangalifu na mavumbi ya soda au kabonati kalisiamu. Osha salio kwa maji mengi. (Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia).
|
Kisichoingiza hewa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Alama: C R: 35 S: (1/2-)-22-26-45 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 8 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 80G03 Msimbo wa NFPA : H 2; F 0; R 2; |
Kinachotenganishwa na dutu zenye kuungua na za kunakisi, vioksidishaji vikali, besi kali, vyakula na malisho, maji. Kavu.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: PODA AU FUWELE YA RISHAI, NYEUPE HATARI ZA KIKEMIKALI: Mmumunyo katika maji ni asidi kali humenyuka vikali ikiwa na besi na husababisha ulikaji. Humenyuka vikali ikiwa na asidi pakloriki kusababisha athari ya moto na mlipuko. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na maji kufanyiza asidi fosforasi. Hushambulia metali nyingi iwapo kuna maji. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki MAK: 1 mg/m³ (1996) |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii husababisha ulikaji kali kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa. Kuvuta pumzi yenye vumbi kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango usablimishaji: 360°C Kiwango myeyuko: 340°C Uzito wiani (maji = 1): 2.4 Umumunyifu katika maji: mmenyuko |
|||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Humenyuka kwa nguvu na vitenzi vya kuzimia moto kama vile maji. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya mnyunyuzio mwafaka unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. KAMWE usimiminie maji dutu hii; wakati wa kumumunyisha au kuzimua, daima itie polepole kwenye maji.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||