PENTACHLOROBENZENE ICSC: 0531
Novemba 2003

1,2,3,4,5-Pentachlorobenzene
CAS # 608-93-5 C6HCl5
RTECS # DA6640000 Masi ya molekuli: 250.3
UN #
EC # 602-074-00-5
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka katika hali mahususi. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)!

Kuvuta pumzi Kikohozi.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru.
Ainisho ya EU
Alama: F, Xn, N
R: 11-22-50/53
S: (2-)-41-46-50-60-61
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
PENTACHLOROBENZENE ICSC: 0531
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE ISO RANGI HADI NYEUPE YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi kama vile kloridi hidrojeni.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru hautafikiwa au utafikiwa polepole sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C wakati wa kunyunyiza au kutawanya, hata hivyo, kwa kasi zaidi.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri ini kusababisha kuharibika kwa ini. Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii huenda ikasababisha athari za sumu kwa uzazi na kukua kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 275-277°C
Kiwango myeyuko: 86°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.8
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 25°C: takribani 2
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 8.6
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.00
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 5.03-5.63
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Kuzidisha kwa kemikali yaweza kutokea kwa samaki, kwa maziwa, kwa mimea na kwa mamalia. Dutu hii inaweza kusababisha madhara yatakayoonekana baadaye katika mazingira ya maji. Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa kuendelea kuwa kwa udongo na kushikilia kwa vidonge kwa maji.
VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005