N-NITROSODIMETHYLAMINE ICSC: 0525
Machi 2001

Dimethylnitrosamine
N-Methyl-N-nitrosomethylamine
DMN
CAS # 62-75-9 C2H6N2O / (CH3)2NN=O
RTECS # IQ0525000 Masi ya molekuli: 74.1
UN # 2810
EC # 612-077-00-3
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka.
Usiwashe moto.
Poda, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kuumwa koo. Kikohozi. Kichefuchefu. Kuhara. Kutapika. Kuumwa kichwa. Udhaifu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Maumivu. Wekundu.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Msokoto wa tumbo. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa.
Ainisho ya EU
Alama: T+, N
R: 45-25-26-48/25-51/53
S: 53-45-61
Angalia: [E]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G61b
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, vyakula na malisho. Baridi. Weka gizani. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
N-NITROSODIMETHYLAMINE ICSC: 0525
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU MANJANO KAMA MAFUTA

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha oksidi za nitrojeni. Humenyuka pamoja na vioksidishaji vikali na besi kali.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: A3, ngozi (ACGIH 2000).
Ainisho ya MAK 2 (2000)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri ini, kusababisha manjano ya macho na ngozi. Athari zinaweza kuchelewa. Tazama Vidokezo. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri ini, kusababisha uharibifu wa utendaji wa ini na ini kuwa gumu (cirrhosis). Dutu hii huenda inasababisha kansa kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 151°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.0
Umumunyifu katika maji: vizuri sana
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 360
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.56
Kiwango cha kumweka: 61°C
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -0.57
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Dalili za manjano hazijitokezi mpaka masaa kadhaa yamepita. Madhara kwa mazingira ya mkabala na dutu hii hayajachunguzwa vya kutosha.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005