| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto.
|
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizo wa maji, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
|
|
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Maumivu ya tumbo. Degedege. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kutapika.
|
Uingizaji hewa (hapana kama ni poda), mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Maumivu. (Tazama Kuvuta pumzi).
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
(Tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Alama: T+ R: 26/27/28 S: (1/2-)-13-28-45 Angalia: [A] Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G67
|
Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, vyakula na malisho.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: MAGAMBA NYEUPE HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu kama vile oksidi za nitrojeni na monoksidi kaboni. Humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji vikali. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho na ngozi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva, kusababisha degedege na kutoweza kupumua. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii huenda ikasababisha athari za sumu kwa uzazi wa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango myeyuko: 90°C Umumunyifu katika maji: vizuri sana |
Jotoridi la kujiwasha: 244°C | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||