NICOTINE ICSC: 0519
Aprili 1997

(S)-3-(1-Methylpyrrolidin-2-yl)pyridine
3-(1-Methyl-2-pyrrolidinyl)pyridine
beta-Pyridyl-alpha-N-methylpyrrolidine
1-Methyl-2-(3-pyridyl)pyrrolidine
CAS # 54-11-5 C10H14N2
RTECS # QS5250000 Masi ya molekuli: 162.2
UN # 1654
EC # 614-001-00-4
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizo wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 95°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 95°C, uingizaji hewa.

MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Mchomo. Kichefuchefu. Kutapika. Degedege. Maumivu ya tumbo. Kuhara. Kuumwa kichwa. Udhaifu. Kizunguzungu. Kutokwa jasho. Kuchanganyikiwa.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Mchomo. (Tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T+
R: 25-27
S: (1/2-)-36/37-45
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G68
Msimbo wa NFPA : H 4; F 1; R 0;
Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, vyakula na malisho. Kavu. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
NICOTINE ICSC: 0519
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KIRISHAI, KISICHO RANGI, CHA MAFUTA, CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HUGEUKA KAHAWIA INAPOFIDULIWA NA HEWA.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu pamoja na oksidi za nitrojeni na monoksidi kaboni. Humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji vikali.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.5 mg/m³ (kama TWA) (ngozi) (ACGIH 1996).
MAK: 0.07 ppm; 0.5 mg/m³ H (1996)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kupitia katika ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho na ngozi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa moyo na mishipa na mfumo mkuu wa neva, kusababisha degedege na kutoweza kupumua. Mfiduo juu zaidi ya OEL huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii huenda ikasababisha athari za sumu kwa uzazi wa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko (hutengana): 247°C
Kiwango myeyuko: -80°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.01
Umumunyifu katika maji: kuchanganyika
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 0.006
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 5.6
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.00
Kiwango cha kumweka: 95°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 240°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 0.7-4
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.2
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Epusha kuingia katika mazingira tofauti na matumizi ya kawaida.
VIDOKEZO
Destruxol, XL All Insecticide ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005