METRIBUZIN ICSC: 0516
Machi 1998

4-Amino-6-tert-butyl-3-methylthio-as-triazin-5-one
4-Amino-6-(1,1-dimethylethyl)-3-(methylthio)-1,2,4-triazin-5(4H)-one
CAS # 21087-64-9 C8H14N4OS
RTECS # XZ2990000 Masi ya molekuli: 214.3
UN # 3077
EC # 606-034-00-8
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka.
Usiwashe moto.
Mnyunyizo wa maji, poda.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi
Uingizaji hewa (hapana kama ni poda), mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi
Glavu za kinga.
Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Kupumzika.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kisha peleka mahala pa usalama.
Ainisho ya EU
Alama: Xn, N
R: 22-50/53
S: (2)-60-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 9
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 90GM7-III
Hifadhi mahali pasipokuwa na unyevu au uchafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
METRIBUZIN ICSC: 0516
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE ZISIO NA RANGI HADI NYEUPE YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa kuzalisha mafusho yenye sumu pamoja na oksidi za nitrojeni na oksidi za sulfuri.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 5 mg/m³ kama TWA; A4 (ACGIH 2005).
MAK haijathibitishwa.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Mfiduo wa viwango vya juu huweza kuleta kudidimia kwa mfumo mkuu wa neva.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: 125°C
Uzito wiani: 1.28 g/cm³
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 0.12
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: <1
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.6
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii huingia katika mazingira kwa matumizi ya kawaida. Utaratibu wa hali ya juu lazima unahitajika ili kuzuia kiasi zaidi kisitokee kama kupitia kwa kutupwa ovyo.
VIDOKEZO
Bay 61597, Bay DIC 1468, Bayer 94337, Bayer 6159H, Bayer 6443H, DIC 1468, Lexone, Sencor, Sencoral, Sencorer, na Sencorex ni majina ya kibiashara.
The cards has been partly updated in April 2005. See sections Environmental Data, EU classification, Occupational Exposure Limits.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005