VINYL TOLUENE (ISOMA ZILIZOCHANGANYIKA) ICSC: 0514
Machi 1996

Methyl styrene (mixed isomers)
Ethenylmethylbenzene (mixed isomers)
CAS # 25013-15-4 C9H10
RTECS # WL5075000 Masi ya molekuli: 118.2
UN # 2618 (imezuiwa)
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua. Ukanzaji unaweza kusababisha ongezeko la kanieneo na kuleta athari ya kupasuka.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, AFFF, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 54°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 54°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO


Kuvuta pumzi Kizunguzungu. Kusinzia. Mazimbwezimbwe. Kuumwa kichwa. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kichefuchefu. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30G35
Msimbo wa NFPA : H 2; F 2; R 1;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi kali, peroksidi, kloridi alumini. Hifadhi iwapo tu imetulia.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
VINYL TOLUENE (ISOMA ZILIZOCHANGANYIKA) ICSC: 0514
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mafusho hayatazuilika na yanaweza kujipolimisha, kuziba kwa matundu na kufuatia.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii kama haijaimarishwa itapolimisha na kutoa joto. Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho na gesi zenye sumu. Dutu hii ni kinakisishaji kikali na humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na chumvi za alumini.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 50 ppm; 242 mg/m³ (kama TWA);
100 ppm; 483 mg/m³ (kama STEL) (ACGIH 1995-1996).
MAK: 100 ppm; 480 mg/m³; (1992).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa neva.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Dutu hii huweza kuathiri ini, kusababisha uharibifu unaoendelea wa shahamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 170-173°C
Kiwango myeyuko: -77°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.90-0.92
Umumunyifu katika maji, g/100 ml: hakuna
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 0.15
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.1
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.00
Kiwango cha kumweka: 45-53°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 489-515°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 0.8-11.0
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 3.58
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Maelezo katika kadi hii yanahusu mchanganyiko wa isoma m- na p-. Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru. Ongezeko la kiimarishaji au kiviza huweza kuathiri tabia ya kitoksini za dutu hii, shauriana na mtaalam.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005