METHYL IODIDE ICSC: 0509
Aprili 2004

Iodomethane
CAS # 74-88-4 CH3I
RTECS # PA9450000 Masi ya molekuli: 142.0
UN # 2644
EC # 602-005-00-9
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO

Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo. Kuumwa kichwa. Kizunguzungu. Kusinzia. Udhaifu. Kuchanganyikiwa. Kuhara. Kichefuchefu. Kutapika. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu. Malengelenge.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T
R: 21-23/25-37/38-40
S: (1/2-)-36/37-38-45
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT1-I
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, vyakula na malisho. Kilichofungwa vizuri. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
METHYL IODIDE ICSC: 0509
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HUGEUKA KAHAWIA INAPOFIDULIWA NA MWANGA NA UNYEVU.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kujilimbikiza katika eneo ambalo dari liko chinichini na kusababisha upungufu wa oksijeni.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa zaidi ya 270C° huzalisha iodidi hidrojeni. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji vikali. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na oksijeni ifikapo 300°C kusababisha athari ya mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 2 ppm kama TWA; (ngozi); (ACGIH 2004).
MAK: Aina ya sarakani: 2 (DFG 2003).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kwa kumeza na kupitia kwenye ngozi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 42.5°C
Kiwango myeyuko: -66.5°C
Uzito wiani (maji = 1): 2.3
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 1.4
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 50
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.9
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 2.9
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.51-1.69
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Dalili za mfumo mkuu wa neva hazijitokezi mpaka masiku au majuma baada ya mfiduo. Hakuna data za kutosha kuhusu athari za dutu hii kwa afya ya binadamu kwa hiyo kunahitajika uangalifu mkubwa.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005