| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua sana.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Poda, AFFF, povu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. Tumia vifaa vya mkono visivyotoa cheche.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kusinzia. Mazimbwezimbwe. Kuumwa kichwa. Kupumua kwa shida. Kuumwa koo. Kupoteza fahamu. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Ngozi kavu. Wekundu. Ukwaru.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kiwaa.
|
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Maumivu ya tumbo. Kichefuchefu. Kutapika. Udhaifu. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Ainisho ya EU Alama: F R: 11 S: (2-)-16-23-29-33 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 3 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 535 Msimbo wa NFPA : H 1; F 3; R 0; |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi. Baridi. Weka gizani. Kilichofungwa vizuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI, CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa inapoathiriwa na hewa, besi, vioksidishaji vikali, UV-mwanga, kusababisha athari ya moto na mlipuko. Dutu hii ni kinakisishaji kikali na humenyuka ikiwa na vioksidishaji. Hushambulia metali nyingi iwapo kuna maji. Hushambulia plastiki. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 200 ppm, 606 mg/m³ (kama TWA); 250 ppm, 757 mg/m³ (STEL) (ACGIH 1997) |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva, kusababisha kupungua kwa fahamu. Mfiduo juu zaidi ya OEL huweza kusababisha kifo. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Kioevu hukausha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri neva za macho, kusababisha kinachorudiarudia upungufu wa kuona. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 57°C Kiwango myeyuko: -98°C Uzito wiani (maji = 1): 0.93 Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 24.4 Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 21.7 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.6 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.3 Kiwango cha kumweka: -13°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 455°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 3.1-16 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.18 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Dalili za uharibifu wa neva za macho hazijitokezi mpaka saa chache ziwe zimepita. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Devoton, Tereton ni majina ya kibiashara.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||