LACTIC ACID ICSC: 0501
Aprili 1997

DL-Lactic acid
2-Hydroxypropanoic acid
alpha-Hydroxypropionic acid
CAS # 50-21-5 C3H6O3 / CH3CHOHCOOH
RTECS # OD2800000 Masi ya molekuli: 90.1
UN #
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka.
Usiwashe moto.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizo wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Mchomo. Kikohozi. Kukosa pumzi. Kuumwa koo.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
Miwanivuli ya usalama, au kingao cha uso.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Msokoto wa tumbo. Maumivu ya tumbo. Mchomo. Kichefuchefu. Kuumwa koo. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Usimpe chochote cha kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Katisha kioevu kilichomwagika kwa uangalifu kwa mmumunyo alkalini dhaifu, mfano kwa kabonati di-sodiamu. Kisha osha kwa maji mengi.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Kinachotenganishwa na besi kali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
LACTIC ACID ICSC: 0501
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KINATACHO, KISICHO RANGI HADI MANJANO AU FUWELE ISO RANGI HADI MANJANO

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii ni asidi kali ya kati.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera ngozi na njia ya upumuaji, na husababisha ulikaji kwa macho. Husababisha ubabuzi inapomezwa.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: 17°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.2
Umumunyifu katika maji: kuchanganyika
Kiwango cha kumweka: 110°C c.c.
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -0.6
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO

MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005