ISOPHORONE DIAMINE ICSC: 0498
Machi 1996

1-amino-3-aminomethyl-3,3,5-trimethylcyclohexane
3-aminomethyl-3,5,5-trimethylcyclohexylamine
CAS # 2855-13-2 C10H22N2
RTECS # Masi ya molekuli: 170.30
UN # 2289
EC # 612-067-00-9
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka.
Usiwashe moto.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizio wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO

Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Inababua. Kuumwa koo. Kikohozi. Mchomo. Kukosa pumzi. Kupumua kwa shida. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Inababua. Maumivu. Wekundu. Malengelenge. Mibabuko ya ngozi. Mchomo.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Maumivu. Wekundu. Kuungua kunakopenya sana. Upofu.
Miwanivuli ya usalama, kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Inababua. Mchomo. Maumivu ya tumbo. Mshtuko au kuzimia. (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: C
R: 21/22-34-43
S: (1/2-)-26-36/37/39-45
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 8
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 647
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, vyakula na malisho. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ISOPHORONE DIAMINE ICSC: 0498
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa na inapochomwa huzalisha gesi zenye sumu na babuzi kama vile oksidi za nitrojeni. Hushambulia shaba, zinki, aloi za stani.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa. Kuvuta pumzi kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 247°C
Kiwango myeyuko: 10°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.92
Umumunyifu katika maji: vizuri sana
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 2
Kiwango cha kumweka: 110°C o.c., 117°C c.c.
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.2-?
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005